Mwandishi Mkuu wa Sheria Bw. Onorius Njole (kulia) akisalimiana na Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Balozi Bishwadip Dey (kushoto) wakati Balozi wa India alipofanya ziara ya kutembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma tarehe 3 Oktoba, 2024.
Mwandishi Mkuu wa Sheria Bw. Onorius Njole (kulia) akifafanua jambo kwa Balozi wa India Mhe. Balozi Bishwadip Dey (kushoto), wakati Balozi huyo alipotembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma.
Mwandishi Mkuu wa Sheria Bw. Onorius Njole (wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Balozi Bishwadip Dey (watatu kutoka kushoto) wakati alipotembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma tarehe 3 Oktoba 2024
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel Maneno (kulia) akisalimiana na Bw. Ng'olo Weja (kushoto) mwakilishi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambaye ni Meneja wa mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati alipotembelea mradi huo Mtumba, Jijini Dodoma
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel Maneno akisisitiza jambo wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma, tarehe 18 Septemba, 2024
Niabu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel Maneno akikagua sehemu ya vifaa vinavyotumika katika mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Divisheni ya Mikataba Bw. Sunday Hyera akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo kuhusu Upekuzi wa Mikataba kwa Mawakili wa Serikali, mafunzo hayo ya siku tano yanafanyika kuanzia tarehe 09 hadi 13 Septemba, 2024. Jijini Dodoma
Kaimu Mkurugenzi wa Divisheni ya Mikataba akifafanua jambo wakati wa Mafunzo ya Upekuzi wa Mikataba kwa Mawakili wa Serikali yanayoendeshwa na Divisheni hiyo, Jijini Dodoma, kuanzia tarehe 09 hadi 13 Septemba, 2024
Wakili wa Serikali Bw. Nyamhanga Nyamhanga akiwasilisha mada kwa Mawakili wa Serikali waliohudhuria Mafunzo kuhusu Upekuzi wa Mikataba yanayoendeshwa na Divisheni ya Mikataba ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Kaimu Mkurugenzi wa Divisheni ya Mikataba Bw. Sunday Hyera (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mawakili wa Serikali walioshiriki katika Mafunzo ya upekuzi wa Mikataba yanayofanyika Jijini Dodoma, kuanzia tarehe 09 hadi 13 Septemba, 2024
Kutoa huduma za kisheria zenye ubora kwa njia ya kuandaa Sheria, Upekuzi na Majadiliano ya Mikataba pamoja na Ushauri wa Kisheria kwa Maendeleo ya Kijamii, Kiuchumi na Kisiasa
Dira
Kuwa Taasisi yenye ufanisi, kitaaluma na kuaminika katika kutoa huduma bora zakisheria kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania