Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani

Majukumu ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani ni moja ya Vitengo katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kitengo hiki kinahusika na Udhibiti wa Matumizi ya Fedha na Raslimali za Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kulingana na taratibu, kanuni na miongozo mbalimbali ya Serikali. Kitengo kinaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kinafanya kazi zifuatazo:

  1.  Kutoa huduma ya uhakiki kwenye shughuli zote zinazofanywa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kupitia kaguzi mbalimbali zinazofanywa kwenye Divisheni na Vitengo husika. Huduma ya uhakiki (Assurance) hizo zimejikita kwenye masuala ya Taratibu za Ndani za Udhibiti, Uendeshaji wa Taasisi na Usimamizi wa Vihatarishi sehemu za kazi, ambazo zimehakikisha utekelezaji mzuri wa majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na mwisho kufikia kwa dira (Vision) na malengo (mission) na misingi (core values) ya Ofisi;
  2. Kupanga, kuratibu na kutekeleza shughuli zinazohusiana na Ukaguzi wa Mahesabu;
  3. kuhakiki mifumo kulingana na udhibiti wa vihatarishi;
  4. Kuandaa taarifa za Ukaguzi wa Ndani na kuwasilisha kwa Afisa Masuuli, Kamati ya Ukaguzi, vitengo husika vinavyokaguliwa;
  5. Kufanya kaguzi maalumu;
  6. Kufuatilia utekelezaji wa ushauri wa taarifa za ukaguzi wa ndani na wa nje; na
  7. Kuandaa Mpango Kazi wa ukaguzi wa Mwaka husika.