Karibu

UKARIBISHO

Kwa niaba ya Menejimenti na Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tunayo furaha kuwakaribisha kwenye tovuti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikiwa na lengo la kuhabarisha na kuelimisha umma na wadau  kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywana Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika juhudi za kuishauri Serikali kwenye masuala ya Kisheria.

Tovuti hii ni nyenzo sahihi itayowezesha umma na wadau kupata habari pamoja na elimu kupitia nyaraka mbalimbali, habari, picha na video ambazo zinapatikana kwaurahisi. Aidha, tovuti hii itatoa fursa kwa umma kupata taarifa mbalimbali na hivyo kuifanya kuwa ni miongoni mwa sehemu muhimu za marejeo katika masuala ya Kisheria.

Natoa wito kwa wadau wote kuendelea kutembelea tovuti hii pamoja na mitandao yetu ya kijamii mara kwa mara na kuwasihi kuwasiliana nasi kwa maoni na, ushauri kwaajili ya kuboresha tovuti yetu, na hata ufafanuzi zaidi juu ya huduma zetu.

Tunawashukuru kwa kuendelea kuiunga mkono Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na tunawakaribisha tena kutembelea tovuti yetu.

Karibuni sana.