TEHAMA (ICT)

Majukumu ya  Kitengo cha TEHAMA (ICT)

Kitengo cha TEHAMA (ICT) ni moja ya Vitengo katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jukumu kuu la Kitengo hiki ni  uendelezaji na uratibu wa Menejiment ya Mifumo ya Komputa   pamoja na  mifumo mengine ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kitengo cha TEHAMA (ICT) kinaongozwa na  Afisa TEHAMA Mkuu.

Kitengo TEHAMA kinatekeleza kazi zifuatazo:-                

  1. Kitengo kinahusika na uendelezaji na uratibu wa Menejimenti ya Mifumo ya Kompyuta pamoja na mifumo mingine ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
  2. Kutekeleza mpango mkakati wa TEHAMA na Serikali Mtandao;
  3. Kuendeleza na kuratibu mifumo ya TEHAMA kwa kushirikiana na Wakala ya Serikali Mtandao;
  4. Kuhakikisha kwamba vifaa na programu za TEHAMA zinasimamiwa na kutunzwa;
  5. Kuratibu na kutoa ushauri katika ununuzi wa programu na vifaa vya TEHAMA;
  6. Kuanzisha na kuratibu matumizi ya mawasiliano ya barua pepe na mitandao;
  7. Kufuatilia na kusimamia usalama wa mifumo ya mawasiliano na taarifa; na
  8. Kusimamia, kufuatilia na kushauri juu ya matumizi ya TEHAMA kama chombo cha kuboresha utoaji wa huduma; na
  9. Kutoa mafunzo kwa watumishi juu ya matumizi sahihi ya TEHAMA.