DIVISHENI YA MIPANGO
Majukumu ya Divisheni ya Mipango
Divisheni ya Mipango ni moja kati ya Divisheni za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Divisheni inahusika na kutoa utaalamu katika maeneo ya Mipango, Utekelezaji wa Bajeti, Ufuatiliaji na Tathmini. Divisheni ya Mipango inaongozwa na Mkurugenzi
Divisheni hii ina sehemu mbili ambazo ni;
- Sehemu ya Mipango na Bajeti;na
- Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathimini
Divisheni ya Mipango inatekeleza kazi zifuatazo :
- Kuandaa na Kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji ya Mwaka kwa Waziri;
- Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Ofisi;
- Kuchambua Sera za Sekta nyingine na kushauri ipasavyo;
- Kuratibu Maandalizi ya Mchango kwenye Hotuba ya bajeti ya Waziri na Taarifa ya kila Mwaka ya masuala ya Uchumi;
- Kujenga Uwezo wa Kuandaa Mpango Mkakati na Bajeti;
- Kufanya Ufuatiliaji na Tathmini ya Mpango na Bajeti ya Ofisi na Kuandaa Taarifa za Utekelezaji;
- Kutathmini Mipango ya Ofisi na Kutoa Ushauri kwa ajili ya Mwelekeo wa Siku zijazo;
- Kuhuisha Mpango na Bajeti ya Ofisi katika Mchakato wa Bajeti ya Serikali;
- Kuratibu Maandalizi na Utekelezaji wa Miradi au Programu za Maendeleo na Ukusanyaji wa Rasimali Zinazohitajika.
- Kuandaa, kutekeleza na kuboresha mpango wa usimamizi wa vihatarishi;
- Kuandaa rejesta ya vihatarishi; na
- Kutoa mwongozo na ushauri ili kuhakikisha kuwa vihatarishi vinatambuliwa, tathminiwa na kupunguzwa.