Uandishi wa Sheria
DIVISHENI YA UANDISHI WA SHERIA
Divisheni ya Uandishi wa Sheria ni moja kati ya Divisheni katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Jukumu kubwa la Divisheni hii ni kuandaa na kuandika Miswaada ya Sheria zote zinazotungwa na Bunge na Sheria ndogo zinazotungwa na Mamlaka mbalimbali. Divisheni hii inaongozwa na Mwandishi Mkuu wa Sheria.
SEHEMU ZA DIVISHENI YA UANDISHI WA SHERIA
Divisheni ya Uandishi wa Sheria ina sehemu tatu (3) ambazo ni:
- Sehemu ya Uandishi wa Sheria
- Sehemu ya Urekebu wa Sheria
- Sehemu ya Fasiri ya Sheria
MAJUKUMU YA DIVISHENI YA UANDISHI WA SHERIA
Kwa mujibu wa Hati ya Idhini ya Maboresho ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Tangazo la Serikali Na.48 la Mwaka 2018 ,Ofisi hii inatekeleza majukumu yafuatayo Kupitia Divisheni ya Uandishi wa Sheria.
- uandishi wa miswada yote ya sheria ya Serikali;
- kushauri katika masuala yote yanayohusiana na mchakato wa utungaji wa sheria;
- kuandaa/kuhakiki sheria ndogo zote zinazotungwa na Wizara na Mamlaka nyingine;
- kuandaa maazimio kwa ajili ya Bunge kuridhia mikataba na Itifaki za kimataifa;
- kufanya urekebu wa sheria kuu na sheria ndogo zote kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Urekebu wa Sheria, Sura ya 4;
- kufanya ufasiri wa sheria kuu, sheria ndogo na nyaraka nyingine za kisheria kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1; na;
- kusimamia utangazaji katika Gazeti la Serikali miswada, sheria kuu na sheria ndogo zote.