Kitengo cha Uhasibu na Fedha

Majukumu ya Kitengo cha Uhasibu na Fedha 

Kitengo cha Uhasibu ni moja ya Vitengo vilivyoko kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kitengo hiki kinahusika na usimamizi wa Fedha na Huduma za Uhasibu unaozintatia  Ubora na Thamani ya Fedha katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kitengo kinaongozwa na Muhasibu Mkuu

Kitango cha Uhasibu kinafanya kazi zifuatazo:

  1. Kushiriki zoezi la Kuandaa mapendekezo na kugawa Fedha za OC kadri zinavyopatikana Kila Mwezi.
  2. Kusimamia, kuandaa na kufanya malipo yote ya ofisi yakiwemo malipo ya watumishi na wazabuni;
  3. Kukusanya maduhuli kwa njia ya Mtandao wa Malipo Serikalini GEPG kwa Kuandaa Kumbukumbu namba ya Malipo (Control number);
  4. Kutunza fedha za ofisi zilizoko ofisi ya malipo (Cash Office) na kuzitoa kwa wahusika au kuzipeleka benki “(deposit”);
  5. Kuandaa taarifa zote za fedha kwa mujibu wa sheria (Annual Financial Statement). Kwa Mwaka wa Fedha unaoishia Juni, 2023, Hesabu zimeshatengenezwa na kuwasilishwa kwa Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mujibu wa taratibu na sheria tarehe 31 Agosti,2023;
  6. Kufanya usuluhishi wa mahesabu (Bank Reconciliation);
  7. Kukagua usahihi na ukamilifu wa nyaraka za malipo;
  8. Kusimamia uandaaji wa majibu ya hoja za ukaguzi;
  9. Kutunza kumbukumbu za kihasibu; na
  10. Kutoa ushauri kwa Menejimenti ya ofisi kuhusiana na masuala ya kifedha.