Mikataba na Makubaliano
Majukumu ya Divisheni ya Mikataba na Makubaliano
Divisheni ya Mikataba na Makubaliano ni moja kati ya Divisheni za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Jukumu kuu la Divisheni hii ni kutoa ushauri na kuendesha majadiliano kwa niaba ya Serikali katika Mikataba yote. Divisheni hii inaongozwa na Mkurugenzi pamoja na Wakurugenzi wasaidizi.
Divisheni hii ina Sehemu Tatu (3), ambazo ni :-
- Sehemu ya Mikataba ya Ununuzi wa Umma
- Sehemu ya Mikataba ya Makubaliano ya Kimataifa
- Sehemu ya Mikataba ya Uwekezaji, Maliasili na Fedha.
Divisheni ya Mikataba na Makubaliano inatakeleza kazi zifuatazo;
- Kuandaa na kutoa ushauri wa kisheria kuhusiana na Mikataba, Hati za Makubaliano na masuala mengine ya Kimkataba yanayoihusu Serikali;
- Kuhakiki, kuratibu na kutoa ushauri wa kisheria kwa Serikali kuhusiana na mikataba ya kikanda na makubaliano baina ya nchi na nchi na mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohusisha Serikali;
- Kutoa ushauri wa kisheria kwa Serikali kuhusiana na majadiliano katika Mikataba inayohusisha Serikali;
- Kufanya utafiti kuhusiana na mikataba mbalimbali ya kimataifa inayotaka kuridhiwa/kuingiwa na Serikali;
- Kutoa ushauri wa kisheria kwa Wizara, Serikali za Mitaa, Idara za Serikali na taasisi nyingine za Serikali na Mashirika ya Umma kuhusiana na Mikataba, Hati za Makubaliano na masuala mengine ya kimkataba yanayoihusu Serikali;
- Kutoa ushauri wa kisheria kwa Wizara, Serikali za Mitaa, Idara za Serikali na taasisi nyingine za Serikali kuhusiana na utekelezaji wa masharti yaliyopo katika mikataba mbalimbali inayohusisha Serikali;
- Kutoa ushauri wa kisheria juu ya uandaaji wa Mikataba, Hati za Makubaliano na masuala mengine yanayoihusu Serikali;
- Kuhakiki na kutoa ushauri wa kisheria kuhusiana na Mikataba ya manunuzi ya umma, mikopo,uwekezaji na rasilimali na uwekezaji inayohusisha Serikali ama taasisi zake