Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (GCU)

Majukumu ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (GCU)

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ni moja ya Vitengo katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, jukumu kuu la Kitengo hiki ni kuhabarisha, kuelimisha na kusimamia masuala yote ya Habari, na Mawasiliano ikiwemo kuhamasisha na kutangaza majukumu na huduma za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kudumisha mahusiano chanya na wadau wake wa ndani na nje. Kitengo hiki kinaongozwa na Afisa Habari Mkuu

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kinatekeleza  kazi zifuatazo:-

  1. Kuratibu kusimamia, kuandaa na kusambaza machapisho vipeperushi, majarida, Magazeti, habari, makala, mabango kwa lengo la kuhabarisha na kuelimisha umma kuhusu utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Ofisi;
  2.  Kuratibu, kusimamia na kufahamisha umma juu ya utekelezaji wa mikutano mbalimbali ya Ofisi ikiwemo mikutano na waandishi wa habari, majadiliano na vyombo vya habari pamoja na kutoa taarifa kwa umma (Press Releases) kuhusu masuala mbalimbali ya Kiofisi;
  3. Kufanya ufuatiliaji (Media Monitoring) wa habari na taarifa mbalimbali zinazoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari (Radio, Televisheni, Magazeti, na Mitandao ya Kijamii) kwa lengo la kuhabarisha watumishi na iwapo itahitajika kutoa ushauri wa kitaalam kwa masuala yanayohusu OMMS;
  4. Kuhamasisha utangazaji wa shughuli za Ofisi kwa ushirikiano na vyombo mbalimbali vya habari kama vile radio, televisheni na, mitandao ya kijamii na maonesho mbalimbali ya kitaifa (Sabasaba, wiki ya Sheria, Wiki ya Kliniki ya Sheria n.k ;
  5. Kuandaa, kuratibu na kutoa taarifa zinazohusu ziara za kikazi na matukio (events) zinazofanywa na Ofisi katika maeneo mbalimbali kwa kuzingatia utekelezaji wa majukumu ya kila siku;
  6. Kuratibu na kushiriki katika mikutano na matukio mbalimbali ya Kiofisi kwa lengo la kuwa na uelewa sahihi juu ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi na kutoa taarifa kwa umma na vyombo vya habari ipasavyo;
  7. Kuratibu na kusimamia uwekaji na uhuishaji wa taarifa mbalimbali katika Tovuti (website) ya Ofisi;(www.oag.go.tz); na
  8. Kutoa ushirikiano katika matukio mbalimbali yanayowahusu wadau hasa vyombo vya habari ili kuimarisha ushirikiano na kujenga mahusiano chanya kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wadau wake.