Uratibu na na Huduma za Ushauri
Majukumu ya Divisheni ya Uratibu na Huduma za Ushauri
Divisheni ya Uratibu na Huduma za Ushauri ni moja ya Divisheni katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Divisheni hii inahusika na Utoaji wa Ushauri wa Kisheria kwa Wizara, Divisheni zinazojitegemea, Wakala, Taasisi za Serikali na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Divisheni inaongozwa na Mkurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi.
Divisheni hii ina sehemu tatu (3) ambazo ni:
- Sehemu ya Uratbu
- Sehemu ya Ushari wa Kisheria
- Sehemu ya Majadiliano na Usimamizi wa Mikataba
Divisheni ya Uratibu na Huduma za Ushauri inatekeleza kazi zifuatazo
- Kutoa Ushauri wa Kisheria kwa Wizara na Taasisi za Serikali
- Kuratibu masuala yote ya sheria katika Taasisi za Serikali na kutoa mrejesho
- Kuratibu kazi za mawakili wote wa Serikali kwa kuhuisha na kutunza kanzi data ya Mawakili wa Serikali na Maafisa wote wanaotekeleza majukumu ya kutoa ushauri wa sheria Serikalin
- Kuhudhuria Vikao vya Kikanda na Kimataifa kila inapohitajika
- Kuhudhuria Vikao cha Majadiliano ya Mikataba mbalimbali yenye maslahi kwa nchi hii inapohitajika.