Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi na Ugavi (PMU)

Majukumu ya Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi na Ugavi (PMU)

Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi na Ugavi (PMU) ni moja ya Vitengo katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kitengo kina wajibu wa kusimamia ununuzi kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 10 ya Mwaka 2023 na kanuni zake za mwaka 2024. Kitengo kinaongozwa na Afisa Manunuzi Mkuu.

Kitengo kinafanya kazi zifuatazo:-

  1. Kusimamia majukumu yote ya Ununuzi na Uuzaji vifaa chakavu kwa njia ya zabuni;
  2. Kusimamia kazi zinazofanywa na zabuni;
  3. Kutekeleza maamuzi ya Bodi ya Zabuni;
  4. Kuandaa Mpango wa Ununuzi na kusimamia utekelezaji wake;
  5. Kutathimini na kuandaa taarifa za mahitaji;
  6. Kuandaa matangazo ya zabuni;
  7. Kuandaa hati ya zabuni na taarifa yake;
  8. Kutoa mikataba iliyoidhinishwa kwa wazabuni;
  9. Kutunza na kuhifadhi kumbukumbu ya ununuzi na uuzaji;
  10. Kuandaa na kuhifadhi rejista ya mikataba ya wazabuni wanaoshinda zabuni;
  11. Kuandaa taarifa za kila wakati zinazofanyika katika stoo kuwezesha uhakiki wa mali na utunzaji wake katika stoo na 
  12. Kuandaa taarifa ya ununuzi ya mwezi, robo mwaka na taarifa ya mwaka