Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu

Majukumu ya Divisheni ya Utawala na Rasilimali Watu

Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu ni moja kati ya Divisheni za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Jukumu kuu la Divisheni hii ni kusimamia utekelezaji wa Sera ya Menejimenti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002 pamoja na Kanuni zake za mwaka 2003. Divisheni hii inaongozwa na Mkurugenzi wa Divisheni. 

Divisheni hii ina sehemu mbili ambazo ni;

  1. Sehemu ya Utawala;na
  2. Sehemu ya Usimamizi wa Rasilimali watu

Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu inatekeleza kazi zifuatazo:-

  1. Kutoa ushauri wa Kitaaluma kwa Menejimenti kuhusu masuala ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu kama vile Ajira za Watumishi;
  2. Mafunzo na Maendeleo, Upandishwaji wa vyeo, usimamizi wa utendaji kazi na maslahi ya watumishi;
  3. Kuwa kiungo kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Tume ya Utumishi wa Umma kuhusu utekelezaji wa Sera ya Ajira na Menejimenti katika Utumishi wa Umma na Sheria mbalimbali za Utumishi;
  4. Kusimamia maandalizi ya bajeti ya mishahara, malipo ya kustaafu na likizo za watumishi;
  5. Kuratibu maandalizi ya malipo ya kustaafu, likizo za watumishi na kuhakikisha makato ya watumishi katika mifuko ya Hifadhi ya Jamiii yametolewa;
  6. Kuratibu masuala ya malalamiko ya watumishi na anuai za jamii (jinsia, Ukimwi na Ulemavu);
  7. Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Mkakati  wa Kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa;
  8. Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja;
  9. Kushughulikia nidhamu na usuluhishi wa migogoro ya Kiutumishi na kutekeleza shughuli za mamlaka ya nidhamu kwa watumishi wa masharti ya kawaida (operational services);
  10. Katibu wa Kamati ya Ajira na vikao vya Menejimenti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
  11. Kusimamia utunzaji wa Kumbukumbu za watumishi na utekelezaji wa Sera ya Kumbukumbu na Nyaraka za kitaifa kuhusu utunzaji wa nyaraka za Serikali;
  12. Kushughulikia maslahi na stahili za Viongozi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na stahili za watumishi;
  13. Kusimamia upimaji na tathmini ya utendaji wa kazi (OPRAS);
  14. Kuendeleza michezo na shughuli za Utamaduni wa Sekretarieti ya Maadili  ya Viongozi wa Umma;
  15. Kusimamia usalama wa ofisi na upatikanji wa vifaa; na
  16. Kusimamia masuala ya Usafirishaji.