TAMASHA LA UFUNGUZI WA MICHEZO YA SHIMIWI
TANGAZO
WATUMISHI WOTE WA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MNAARIFIWA KUWA SHIRIKISHO LA MICHEZO YA WIZARA NA IDARA ZA SERIKALI (SHIMIWI) LIMEANDAA TAMASHA LA UFUNGUZI WA MICHEZO YA SHIMIWI LITAKAYOFANYIKA TAREHE 20 AGOSTI, 2022 JIJINI DODOMA LENYE KAULI MBIU YA ‘MICHEZO NI AFYA KWA MAENDELEO YA TAIFA …… JIANDAE KUHESABIWA TAREHE 23 AGOSTI, 2022.
BONANZA HILO LITAFANYIKA KATIKA UWANJA WA JAMHURI LIKITANGULIWA NA JOGGING KUANZIA VIWANJA VYA BUNGE NA KUFUATIWA NA MICHEZO YA MPIRA WA MIGUU, KAMBA NA NETIBOLI. MGENI RASMI ATAKUWA MKUU WA WATUMISHI WA UMMA KATIBU MKUU KIONGOZI MHE. BALOZI HUSSEIN KATANGA.
OFISI IMEANDAA USAFIRI WA BASI COASTER NAMBA S.T.L 8450 KWA AJILI YA KUBEBA WATUMISHI KUTOKA IPAGALA KWENDA UWANJA WA JAMHURI. BASI LITAONDOKA IPAGALA SAA 12:30 ASUBUHI, HIVYO WATUMISHI WOTE MNASISITIZWA KUHUDHURIA KATIKA BONANZA HILO BILA KUKOSA.
IMETOLEWA NA,
UTAWALA
19/08/2022