Upekuzi wa Mikataba
DIVISHENI YA MIKATABA NA MAKUBALIANO YA KIMATAIFA
Divisheni hii inahusika na kutoa Ushauri na kuendesha Majadilano kwa niaba ya Serikali katika Mikataba yote.
MAJUKUMU YA DIVISHENI YA MIKATABA
- Uhakiki wa Mikataba ya Manunuzi
- Uhakiki wa Makubaliano ya Kitaifa na Kimataifa
- Kuhudhuria na kutoa mapendekezo ya nchi katika vikao vya kikanda na kimataifa kwa maslahi ya nchi
- Kuhudhuria Vikao vya Majadiliano ya Mikataba mbali mbali yenye maslahi kwa nchi kila inapohitajika;na
- Kutoa Ushauri kwenye Mikataba ya Mikopo
SEHEMU ZA DIVISHENI YA MIKATABA
Divisheni ina Sehemu Tatu (3)vinavyoongozwa na Wakurugenzi Wasaidizi. Sehemu hizo;
- Sehemu ya Mikataba ya Ununuzi wa Umma
- Sehemu ya Mikataba na Makubaliano ya Kimataifa
- Sehemu ya Mikataba ya Uwekezaji, Maliasili na Fedha