OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAKAMILISHA MRADI WA UREKEBU WA SHERIA NCHINI. 

Imewekwa: 23 Apr, 2025
OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAKAMILISHA MRADI WA UREKEBU WA SHERIA NCHINI. 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari amesema kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekamilisha zoezi la urekebu wa sheria mbalimbali nchini. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ameyasema hayo akizungumza katika kipindi cha Jambo cha TBC Jumanne tarehe 22 Apili, 2024. 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema mradi wa urekebu wa sheria umefanyika kwa lengo la kujumuisha marekebisho ya sheria mbalimbali zilizopitishwa na bunge kuwa kitu kimoja ili kuwarahisishia watumiaji wa sheria hizo.

Aidha, Mhe. Johari amesema utekelezaji wa mradi wa zoezi la urekebu wa sheria umefanyika kwa kutumia rasilimali za ndani, ambapo Serikali imetoa fedha na pamoja kuendelea kuijengea uwezo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuwazesha watumishi wa Ofisi hiyo kushiriki kwenye mafunzo mbalimbali ya uandishi wa Sheria.

“Mradi huu kwa mara ya kwanza unafanyika kwa kutumia rasilimali zetu za ndani, tumeweza kujenga uwezo wetu kwa kuhakikisha kuwa tuna rasilimali fedha za kutosha na watumishi wa kutosha.” Amesema Mhe. Johari

Vilevile Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kuwa zoezi la urekebu limehusisha majumuisho ya jumla ya sheria kuu 446 ambazo zitakuwa zinapatikana katika jumla ya majuzuu 20 ili kurahisisha watumikaji. 

“Jumla ya sheria kuu 446 zimefanyiwa majumuisho na tunatarajia kuzipata sheria hizi katika juzuu za sheria 20 kwa lengo la kuwarasishia watumiaji wa sheria husika.” Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali 

Katuka hatua nyingine Mhe. Johari amesema kuwa kukamilia kwa zoezi la urekebu wa sheria litasaidia katika ukuaji wa uchumi, upatikanaji wa haki madai na haki jiani pamoja na kuwarahishia wasomaji wa sheria kwakuwa sheria zilizofanyiwa zitakuwa zikipatikana kirahisi. 

Juzuu za Sheria zilizofanyiwa urekebu zinatarajia kuanza kutumika mara baada ya kutolewa kwa tamko rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.