Ushauri wa Kisheria
DIVISHENI YA URATIBU NA HUDUMA ZA USHAURI
Divisheni ya Uratibu na Huduma za Ushauri ni moja ya Divisheni katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Divisheni hii inahusika na Utoaji wa Ushauri wa Kisheria kwa Wizara, Divisheni zinazojitegemea, Wakala, Taasisi za Serikali na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Divisheni inaongozwa na Mkurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi.
SEHEMU ZA DIVISHENI ZA URATIBU NA HUDUMA ZA USHAURI
Divisheni hii ina sehemu tatu (3) ambazo ni:
- Sehemu ya Uratibu
- Sehemu ya Ushari wa Kisheria
- Sehemu ya Majadiliano na Usimamizi wa Mikataba
MAJUKUMU YA DIVISHENI YA URATIBU NA HUDUMA ZA USHAURI
Divisheni ya Uratibu na Huduma za Ushauri inatekeleza kazi zifuatazo
- Kuratibu usimamizi wa Maafisa Sheria, Mawakili wa Serikali, na wafanyakazi wengine wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara, Taasisi za Serikali, Wakala wa Serikali na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
- Kutunza na kuhuisha kansi data ya Maafisa wa Sheria, Mawakili wa Serikali na waajiriwa wengine katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara, Taasisi za Serikali, Wakala wa Serikali, Mamlaka za Serikali za Mitaa na kushauri ipasavyo.
- Kuratibu na kusimamia utoaji wa ushauri wa kisheria kwa mujibu wa mamlaka iliyonayo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ikiwemo kusimamia maamuzi na mrejesho kwa kuratibiwa na Divisheni ya Mikataba na Makubaliano ya Kimataifa.
- Kupanga na kusimamia utafiti wa kisheria katika masuala magumu ya kisheria, kuandaa ushauri wa kisheria, tafiti, Mihutasari, taarifa na mawasiliano.
-
Kufanya tafiti za kisheria kwenye mambo yote yanayoletwa katika Divisheni ya Uratibu na Huduma za Ushauri wa Kisheria kwa ajili ya kutolewa ushauri wa kisheria;
-
Kutoa ushauri kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wakala, Wananchi, Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali juu ya masuala yote yanayohusu sheria;
-
Kuanzisha na kutunza kanzi data na taarifa/ kumbukumbu za ushauri wote unaotolewa na Divisheni kwa Wizara, Taasisi, Wakala Mashirika ya Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa;
-
Kushiriki na kushauri katika majadiliano ya mikataba ama miradi ambayo Serikali ina maslahi;
-
Kushiriki na kushauri katika majadiliano ya utatuzi wa migogoro ya mashauri au nia za kufungua mashauri katika mabaraza na Mahakama mbalimbali; na
-
Kushauri katika utekelezaji wa mikataba iliyoingiwa na Serikali;