TANGAZO KWA MAWAKILI WA SERIKALI
ZOEZI LA KUPITIA TAARIFA ZA MAWAKILI WOTE WA SERIKALI ZILIZO
KATIKA MFUMO WA OAGMIS LINAENDELEA ILI KUJIRIDHISHA NA VIGEZO
VYA KUWA WAKILI WA SERIKALI NA KUHUISHA NAMBA ZA
UTAMBULISHO WA MAWAKILI WA SERIKALI.
BAADHI YA CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA NI:
1. BAADHI YA MAJINA YA VYEO KUTOAKISI MOJA KWA MOJA
MAJUKUMU YA UTOAJI WA HUDUMA ZA KISHERIA KWENYE
UTUMISHI WA UMMA;
2. MAWAKILI WA SERIKALI KUTOAMBATISHA BARUA
ZINAZOWAONESHA KUAJIRIWA KATIKA NAFASI ZENYE KUWA NA
MAJUKUMU YA UTOAJI WA HUDUMA ZA KISHERIA; na
3. MAWAKILI KUTOKAMILISHA KUJAZA BAADHI YA TAARIFA ZAO
MUHIMU.
ZOEZI LITAKAPOKAMILIKA, ORODHA YA MAWAKILI WA SERIKALI
WENYE SIFA NA VIGEZO PAMOJA NA NAMBA MPYA ZA MAWAKILI WA
SERIKALI ZITAPATIKANA KWENYE KIKOA CHA oagmis.agctz.go.tz.
WITO KWA MAWAKILI WA SERIKALI
- KUKAMILISHA TAARIFA MUHIMU KWENYE MFUMO WA OAGMIS.
- KUWEKA BARUA ZINAZOONESHA ULIPOANZA KUTEKELEZA MAJUKUMU KAMA MWANASHERIA KWENYE UTUMISHI WA UMMA.
KWA CHANGAMOTO YEYOTE WASILIANA NASI KWA SIMU KUPITIA :
+255 686 701 313
+255 753 818 910
+255 676 216 002
ASANTE