WATUMISHI WAPYA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA MISINGI YA WELEDI NA UBORA

Imewekwa: 27 Nov, 2025
WATUMISHI WAPYA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA MISINGI YA WELEDI NA UBORA

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel M. Maneno amewataka Watumishi wapya na waliohamia katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuzingatia misingi ya Weledi na Ubora wakati wa kutekeleza majukumu yao, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo alipokutana na kufanya kikao na Watumishi hao tarehe 27 Novemba, 2025 Jijini Dodoma.

Akizungumza katika kikao hicho Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali amewataka Watumishi hao kuisoma na kuelewa Dira na Dhima ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambayo ni moja ya muongozo unaotumika katika kutekeleza majukumu mbalimbali.

 “Niwaombe kila mmoja wenu asome na kuipitia Dira na Dhima ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuelewa nini anatakiwa kufanya ili kutekeleza Dira na Dhima yetu” Amesema Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Aidha, Mhe. Maneno ameeleza kuwa ni muhimu kwa Watumishi hao kuiishi kauli mbiu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Weledi na Ubora, ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kupelekea kutimiza malengo ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

“Wakati wa kutekeleza majukumu yetu ni vyema tukazingatia kauli mbiu yetu ya Weledi na Ubora kwakuwa matarajio yetu kila mmoja afanye kazi katika hali ya Ubora na zenye Weledi wa hali ya juu”. Amesisitiza Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Vilevile Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali amewasisitizia Watumishi hao kuzingatia Maadili ya Msingi ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ubunifu, Uadilifu, Uwazi, Uwajibikaji na Ushirikiano ambapo ameeleza kuwa kwa kufuata maadili hayo itawasaidia watumishi hao katika utendaji wa majukumu yao ya kila siku. 

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametumia Kikao hicho kuwakaribisha Watumishi wapya na waliohamia katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kueleza kuwa ana matarajio makubwa kutoka kwa watumishi hao katika kuboresha utendaji kazi wa Ofisi hiyo