The United Republic of Tanzania
The Office of the Attorney General

PRIME MINISTER HON. DR. MWIGUL...

PRIME MINISTER HON. DR. MWIGULU LAMECK NCHEMBA LED THE FUNERAL MASS FOR LATE HON. LUKUVI.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani Mhe. William Vangimembe Lukuvi (Mb) katika Viwanja vya Bunge, jijini Dodoma tarehe 27 Machi, 2026.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe Hamza S. Johari ni miongoni mwa Viongozi wa Serikali waliohudhuria Misa hiyo kutoa heshima za mwisho katika Viwanja vya Bunge, Jijini Dodoma.

Mhe. Lukuvi alifariki tarehe 25 Machi, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa ,Jijini Dodoma, alipokuwa akipatiwa matibabu.