MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MHE. HAMZA S. JOHARI AAPISHWA KUWA MBUNGE

Imewekwa: 11 Nov, 2025
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MHE. HAMZA S. JOHARI AAPISHWA KUWA MBUNGE

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amekula kiapo cha Uaminifu mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Musa A. Zungu, tarehe 11 Novemba, 2025. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameapishwa kuwa Mbunge  katika  kikao cha kwanza cha Mkutano wa kumi na tatu(13)  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameapishwa kwa mujibu wa Ibara ya 59(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 inayompa Mamlaka ya kuwa Mbunge na kuhudhuria vikao vya Bunge.

Aidha, Uapisho huo mbele ya Bunge wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  unafuatia Uteuzi   uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kumteua Mhe. Hamza  S. Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali mnamo tarehe 3 Novemba, 2025 na kufuatiwa na uapisho uliofanyika tarehe 5 Novemba, 2025 Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma.