MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AKUTANA NA UONGOZI WA TLS NA KUHIMIZA USHIRIKIANO  KATIKA KUWATUMIKIA WATANZANIA 

Imewekwa: 01 Nov, 2024
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AKUTANA NA UONGOZI WA TLS NA KUHIMIZA USHIRIKIANO  KATIKA KUWATUMIKIA WATANZANIA 

Akizungumza katika kikao  kilichowakutanisha  Uongozi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) na Menejimenti  ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari amesema kuwa, TLS ni mdau muhimu katika kuishauri Serikali kwa kubaini mambo muhimu yaliyopo katika utekelezaji  wa Sheria mbalimbali Nchini na hivyo ujio huo ni hatua muhimu katika kuimarisha mahusiano baina ya pande hizo mbili. 

Mwanasheria Mkuu ameyasema hayo Leo tarehe 1 Novemba, 2024   ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma wakati alipofanya  mazungumzo na Uongozi wa TLS  walipofika kwa ajili ya kujitambulisha, kufahamiana na kuboresha mahusiano baina ya Ofisi hizo. 

"TLS ni mdau wetu mkubwa hivyo tunathamini sana ujio wenu na tunaamini itaongeza wigo wa ushirikiano katika utendaji kazi"Alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 

Rais wa  TLS Wakili Boniphace Anyisile Kajunjumele Mwabukusi  amesema TLS inaiona  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni nyumbani hivyo pande hizi  mbili zinapaswa  kushirikiana kwa maslahi ya Wanasheria na Taifa.  

"Tunapenda TLS ifanye kazi kwa maadili Uwakili wetu uwe credible tunaweza kushindana na kuvutia watu wa au aina tofauti tofauti kwa kuzungumza na kuimarisha Sheria kwa manufaa ya Taifa letu."Alisema Rais wa TLS 

Kwa upande wake Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel Maneno amesema, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  kwa sasa imepiga hatua kubwa katika matumizi ya mifumo mbalimbali ili kuimarisha na  kurahisisha  utekelezaji wa majukumu yake ikiwa ni pamoja na mfumo wa  OAG-MIS  unaowezesha  upatikanaji wa Sheria mbalimbali pamoja na Sheria zote zilizofanyiwa  Marekebisho. 

Aidha,  Naibu Mwanasheria Mkuu amemuomba Rais wa TLS kutumia majukwaa yao kutangaza mafanikio ya mfumo hu