The United Republic of Tanzania
The Office of the Attorney General

Legal Advisory Committee Launc...

Legal Advisory Committee Launched in Manyara

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa

Kutumia Mawakili na Wanasheria wenye Weledi katika utatuzi wa kesi mbalimbali ili changamoto zao zitatuliwe kwa wakati.

Hayo yameelezwa Leo na Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, wakati akizindua Kamati ya Ushauri wa Kisheria ngazi ya Mkoa na Wilaya na Kliniki ya Sheria bila malipo ambayo imefanyika wilayani Hanang mkoani Manyara na kuwataka wananchi kutumia kliniki hiyo kuelezea changamoto zao za Kisheria.

Vilevile Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, ameipongeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa Kuandaa huduma ya Kisheria kwa Wananchi wa Mkoa wa Manyara.

“Niishukuru Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwa msaada wa Huduma za Kisheria katika Mkoa wa Manyara, hususan Wilaya ya Hanang, nina matumaini Wananchi wa Mkoa wa Manyara, watapata utatuzi wa changamoto zao za Kisheria” Amesema Mhe. Queen Sendiga

Awali akifanya utambulisho, Mkurugenzi wa Uratibu na Huduma za Ushauri kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Neema Ringo, amesema kamati hizi zimeanza kufanya kazi kuanzia Januari 19 hadi Januari 25 ambapo Zaidi ya Mawakili 30 wapo wilayani Hanang kutoa huduma ya Kisheria.

Mbunge wa jimbo la Hanang Asia Halamga ameeleza wilaya ya Hanang ni wilaya yenye changamoto kubwa za migogoro ya Ardhi , hivyo kupitia Kliniki hii wananchi wengi watapata msaada wa Kisheria.

Aidha, baadhi ya wananchi ambao wameudhuria katika kliniki hiyo, wameishukuru serikali kwa kutoa msaada wa kisheria Bure kwani kliniki hiyo itasaidia kutatua changamoto zao.

Uzinduzi wa Kamati ya Ushauri Ngazi ya Mkoa na Wilaya umefanyika leo tarehe 20 Januari, 2026, na Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, Mkuu wa Mkoa wa Manyara.