TANGAZO LA UCHAGUZI WA VIONGOZI  WA CHAMA CHA MAWAKILI WA SERIKALI (PUBLIC BAR ASSOCIATION)

Imewekwa: 17 Feb, 2024 Pakua

TANGAZO LA UCHAGUZI WA VIONGOZI

 CHAMA CHA MAWAKILI WA SERIKALI (PUBLIC BAR ASSOCIATION)

----------------------

UTANGULIZI

Chama Cha Mawakili wa Serikali (PBA) kimeanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 16A(1) cha Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Sura 268 na Tangazo la Serikali Na. 589 la tarehe 16 Agosti 2019.

Uongozi wa Mpito wa Chama cha Mawakili wa Serikali unapenda kuwajulisha wanachama wake wote wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama, kuzingatia utaratibu ulioainishwa katika Tangazo hili kwa ajili ya kugombea nafasi husika, kama ifuatavyo:

  1.  UONGOZI

Nafasi za Uongozi zinazogombewa ni:

  1. Rais (Doyen)
  2. Makamu wa Rais (Deputy Doyen)

Sifa za Wagombea wa Nafasi ya Uongozi

Mwanachama mwenye nia ya kugombea nafasi mojawapo katika hizi, anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:

  1. Wakili wa Serikali/Afisa Sheria aliyesajiliwa kwenye mfumo wa OAGMIS na kupatiwa Roll Number kwa mujibu wa sheria, Sura 268 na kuwa Mwanachama wa Chama cha Mawakili wa Serikali; na
  2. Wakili wa Serikali/Afisa Sheria mwenye cheo kuanzia Wakili wa Serikali/Afisa Sheria Mwandamizi na kuendelea (Law Officer).

 

  1. KAMATI YA UTAWALA

Nafasi zitakazogombewa katika kamati hii ni zifuatazo:

  1. Mwenyekiti;
  2. Makamu Mwenyekiti;
  3. Katibu;
  4. Mweka Hazina; na
  5. Mjumbe mmoja kutoka kila mkoa atakayechaguliwa na wanachama kutoka katika mkoa husika.

Sifa za Wagombea Nafasi ya Kamati

Wakili wa Serikali/Afisa Sheria aliyesajiliwa kwenye mfumo wa OAGMIS na kupewa Roll Number kulingana na Sheria, Sura 268, na kuwa Mwanachama wa Chama cha Mawakili wa Serikali.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAGOMBEA WOTE

  1. Kila mgombea kwa nafasi yoyote anapaswa kudhaminiwa na wanachama wasiopungua watano (5);
  2. Mgombea/mpiga kura lazima awe aliyesajiliwa kwenye mfumo wa OAGMIS na kupewa Roll Number kulingana na Sheria, Sura 268, na kuwa Mwanachama wa Chama cha Mawakili wa Serikali;
  3. Fomu zinapatikana kwenye Tovuti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali au OAGMIS;
  4. Fomu zote ziwasilishwe kwa Katibu wa Kamati, Bi Sia B. Mrema kupitia barua pepe sia.mrema@agctz.go.tz nakala kwa Mwenyekiti Bw. Stephano Mbutu  kupitia barua pepe stephano.mbutu@madini.go.tz; na
  5. Fomu zitakazowasilishwa nje ya muda uliowekwa hazitafanyiwa kazi.

RATIBA YA UCHAGUZI

1. 20/02/2024-27/02/2024-Kuchukua na kurudisha Fomu;

2. 29/02/2024-10/03/2023-Vikao vya kuchuja Wagombea;

3. 11/03/2024-Majina ya wagombea waliopitishwa kutangazwa; na

4. 12/03/2024-21/03/2024-Kampeni kwa wagombea waliopitishwa.

 

Kwa mawasiliano tafadhali wasiliana na:

Bi. Juliana Changarawe: +255 788 473707

Bw. Kadete Mihayo:            +255 716 893 585

Bi.  Jenipher Kaaya:      +255 715778999

Bw. Reward Mriya:              +255 758 906 875

Bw. Ludovick Ringia:           +255 714 560 460

 

SIA MREMA

KATIBU

16/02/2024