TANGAZO KWA WANACHAMA WA PBA
Chama cha Mawakili wa Serikali (PBA) na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) vinashirikiana katika kufanya mapitio ya taarifa za Mawakili wa Serikali ambao pia ni wanachama wa TLS. Lengo la zoezi hilo ni kubaini wanachama wanaopaswa kulipiwa ada za vyama hivyo kuanzia tarehe 1 Julai, 2023 kutoka kwa Maafisa Masuuli wao kufuatia maelekezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyoyatoa tarehe 10 Novemba, 2022.
Zoezi hili linafanyika kupitia Mifumo ya OAGMIS na Wakili Database ambapo hadi kufikia tarehe 30 Mei, 2023, taarifa zinaonesha kuwa PBA ina jumla ya wanachama 3038 ambapo kati yao, wanachama 951 pia ni wanachama wa TLS. Uchambuzi zaidi unaonesha kuwa takwimu hizi haziakisi uhalisia kutokana na changamoto mbalimbali hususani kuwepo kwa tofauti ya taarifa za mawakili katika mifumo hii miwili.
Katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo, ni vema Wakili wa Serikali ambaye jina lake halipo kwenye orodha iliyoambatishwa na tangazo hili awasilishe namba yake ya Usajili wa Uwakili (Roll of Advocates) kwenye mfumo wa OAGMIS kupitia kwa Afisa Utumishi (Focal Person) anayehusika ofisini kwa mwajiri wake.
Mwisho wa zoezi la kuhuisha taarifa hizo kwa wakili mmoja mmoja ni tarehe 9 Juni, 2023. Hatua hii itawezesha PBA na TLS kuwatambua wanachama halisi kwa kila chama na kuwasilisha orodha ya wanachama kwa Maafisa Masuuli wote nchini ili kuwawezesha kutekeleza maelekezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa wepesi ndani ya robo ya kwanza ya mwaka mpya wa fedha.
Nawatakia utekelezaji mwema.
Sia B. Mrema
Katibu - Kamati Tendaji
30 Mei, 2023