Waziri Mkuu azindua Miongozo ya Sheria
Imewekwa:
23 Mar, 2024

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amezindua Miongozo ya Sheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambayo itatumiwa na Mawakili wote wa Serikali kutoka katika Wizara, Mamlaka na Taasisi mbalimbaliza Serikali katika kutekeleza majukumu yao.
Uzinduzi huo umefanyika kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali wa Tanzania wa mwaka 2024 uliofanyika tarehe 22 Machi, 2024 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Conventions Centre Jijini Dodoma. Pamoja naye ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (kulia) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt Eliezer Feleshi (kushoto)