WATUMISHI 80 WA OMMS WAPATIWA KOMPYUTA MPAKATO

WATUMISHI 80 OMMS WAPATIWA KOMPYUTA MPAKATO
Na Mwandishi wetu
MTUMBA-Menejimenti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kikao chake kilichoketi chini ya Uenyekiti wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa kimepitisha mgao wa Kompyuta Mpakato kwa watumishi 80
Kikao hicho kimefanyika leo (Ijumaa) katika ukumbi wa Mikutano Mtumba ambapo kabla mgawanyo huo Mwenyekiti alitoa maelezo mafupi yakiwamo ya namna vifaa hivyo vya TEHAMA vilivyopatikana na mgawayo wake ambao umezingatia masuala kadhaa.
“Ndugu wajumbe tumekutana leo katika kikao hiki kama menejimenti ili tuweze kujadiliana na kupitisha mgao wa komputa mpakato ambazo kati yake ni zile ambazo Ofisi ilikabidhiwa na Mhe. Rais na nyingine zinatokana na Mradi wa BSAAT”. Akaeleza Mwenyekiti
Akaeleza kwamba, mchanganuo wa ugawaji vifaa hivyo umezingatia mambo kadhaa ambayo ni Tange la Watumishi wa Ofisi, mahitaji kutokana na majukumu ya kila siku ya watumishi husika na waajiriwa wapya hasa mawakili wa Serikali .
Dkt Longopa akaeleza Zaidi kwamba, watumishi ambao hawapo kwenye mgao huu na pia hawana vifaa hivyo vya TEHAMA pamoja na baadhi ya Vitengo watapewa kipaumbele katika mgao utakaofuta.
Aidha Watumishi watatu ambao wapo kwenye masomo ya muda mrefu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutoka Divisheni za Mikataba na Uratibu hawakuzingatiwa katika mgao huo kwa wakati huu kwa kuwa wapo masomoni.
Menejimenti imepitisha mgao huo kwa Divisheni na Vitengo pamoja na majina ya watumishi watakaopatiwa vifaa hivyo kama ifuatavyo;
1.Divisheni ya Utawala watumishi wanne ( Laptop 4),
2. Divisheni ya Mikataba watumishi 25( Laptop 25),
3.Divisheni ya Uandishi wa Sheria Watumishi 26 ( laptop 26),
4.Divisheni ya Uratibu na Ushauri wa kisheria watumishi 21 ( Laptop 21),
5.Divisheni ya Mipango watumishi wawili ( laptop 2),
5.Kitengo cha Uhasibu Watumishi wawili ( Laptop2),
6.Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani watumishi 2(laptop 2),
7.Kitengo cha Tehama watumishi wanne ( Laptop4)
Vile vile Menejimenti ilipitisha mgao wa kumpyuta za Mezani tatu (3) kwa Divisheni ya Mikataba(1), Uratibu (1) na Utawala (Dar) 1.
Aidha Printer cum Scanner ziligawiwa kwa DCT 1,CPD 1 na Masjala ya siri1. Pia CPD wamepewa Heavy Duty Printer 1.
Maelekezo ya Menejimenti ni kwamba kwa watumishi waliopo mikoani na ambao ni ajira mpya utaratibu utafanyika wa kuwafikishia vifaa hivyo. Jumla ya Mawakili wa Serikali wapya 39 watakuwa wamepatiwa vitendea kazi hivyo kwa mgawanyo wa CPD 10, DCAS15 na DCT 14.
Pamoja na waajiriwa hao wapya kutoka Divisheni hizo kupatiwa vitenda kazi, Menejimenti ilielezwa kwamba bado kutakuwa na upungufu wa vitenda kazi hivyo kwa Mawakili 16 kutoka DCAS na DCT ambao watafikiriwa katika awamu inayokuja.
Aidha kwa Mujibu wa Mwenyekiti kwa upande wa CPD ambao wanafanya zoezi la urekebu baada ya mgao huu Waadishi wa Sheria wote watakuwa na kumpyuta mpakato.
Aidha kila Mkuu wa Divisheni na Kitengo ameelekezwa kusimamia zoezi la ugawaji wa vifa hivyo kuanzia leo Ijumaa kwa watumishi ambao wapo chini yao kwa kuwasainisha kila mmoja anayekabidhiwa kifaa hicho
Vile vile menejimenti imesisitiza umuhimu kwa watumishi wote wa kuwa na matumizi sahihi ya vifaa hivyo hasa katika kipindi hiki ambacho Taasisi inatekeleza majukumu yake kupitia mifumo ya Taarifa wa Kielektroniki wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ( OAG-MIS) pamoa na Mfumo wa Mawasiliano ya Serikali Mtandao (e-Office) Aidha suala la utunzaji na uhifadhi salama wa vifaa hivyo limesisitizwa kwa kila mtumishi.
Ikumbukwe pia kwamba upatikanaji wa vifaa vya Kisasa vya TEHAMA kwaajili ya watumishi na Ofisi kwa ujumla umetokana na kwa kiasi kikubwa Juhudi na jitihada za kubwa zinazofanywa na Mkuu wa Taasisi yetu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano
26/5/2023