OMMS YAASWA KUZINGATIA VIASHIRIA HATARISHI KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAKE

Imeelezwa kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inapashwa kuhakikisha kwamba, udhibiti wa viashiria hatarishi unakuwa sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya .
Hayo yameelezwa hivi karibuni na Bw. Elias Madafu kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe wakati wa mafunzo ya siku mbili ( Octoba 24/25) ya kuwajengea uelewa wa Pamoja Risk Champions kutoka Divisheni na Vitengo kuhusu Pamoja na mambo mengine suala zima la maeneo gani yanaweza kuwa hatarishi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya OMMS.
Bw. Madafu aliwaeleza washiriki hao kwamba , kama Risk Champions wanaowajibu wa kuagalia au kubaini ni viashiria gani hatarishi ambavyo vinaweza kutokea wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kiofisi na ambavyo vinaweza kusababisha Ofisi ikashindwa kutekeleza mipango yake na kufikia malengo iliyojiwekea.
“ Baada ya kujua viashiria hatarishi, unatafuta namna ya kukabiliana navyo. Hii itasaidia Ofisi kufikia malengo yake na kupunguza gharama ambazo zingetokea ikiwa viashiria hivyo visingeshughulikiwa mapema” akasisitiza Bw. Magafu
Na kuongeza. “Ni wajibu wa kila mtumishi wa OMMS kuhakikisha anatengeneza mazingira rafiki na wezeshi ili kuifanya Ofisi iendelee kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kwa kuzingatia taalama yao na weledi
Kwa mujibu wa Divisheni ya Mipango na ambayo ndiyo iliyoandaa mafunzo hayo inaeleza kuwa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli Miramonti, Dodoma. washiriki waelimishwa na kujengewa uwezo kuhusu Mfumo wa Viashiria Hatarishi pamoja na kuangalia Rejesta ya Vihatarishi katika kila Divisheni na Vitengo vyao na pia kuboresha nyaraka zilizohuishwa kwenye mafunzo ya awali ya Divisheni ya Mipango.
Divisheni ya Mipango katika taarifa yake inasema mafunzo yaliyotolewa kwa Risk Champions hao ni muendelezo baada ya hatua ya awali iliyohusisha Wataalam wa Divisheni walipojengewa uelewa wa Pamoja wa namna ya kuandaa na kuhuisha nyaraka za Mfumo wa Usimamizi wa viashiria hatarishi (Risk Management Framework) na Rejesta ya Viashiria Hatarishi (Risk Register) ya OMMS.
Mwisho
27/10/2023