OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAWAPIGA MSASA MAWAKILI SERIKALI
Imewekwa:
12 Jun, 2024

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliratibu na kuendesha mafunzo kwa Mawakili wa Serikali.
Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo Mawakili kwenye masuala mbalimbali yanayohusu sheria ikiwemo Uandishi wa sheria, mambo muhimu ya kuzingatia kwenye Mikataba na Makubaliano baina ya Nchi au Taasisi, pamoja na mambo ya kuzingatia katika kuishauri Serikali kwenye nyanja ya Sheria.
Mafunzo hayo yalifanyika Jijini Dodoma hivi karibuni na kuhudhuriwa na Mawakili takribani mia mbili na tisini (290) kutoka taasisi mbalimbali za Serikali.