NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA BENKI YA TCB PLC

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Samweli M. Maneno amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Benki ya TCB Plc, Alhamis tarehe 17 Aprili, 2025 katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Ujumbe huo ulitembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa lengo la kujitambulisha na kuelezea huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akiwemo Mkurugenzi wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bi. Faith Minani, Kaimu Mkurugenzi wa Divisheni ya Mikataba na Makubaliano, Bi. Mukabatunzi Rwakilomba na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi. Leila Muhaji.
Ujumbe kutoka TCB plc umeongozwa na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bw. Dotto Kahabi ambaye aliambatana na Meneja Mkuu wa Huduma za Sheria, Bi. Marydensia Katemana, Meneja wa Tawi la Capital Dodoma Bi. Asia Mwangonela pamoja na Meneja wa Mahusiano - Taasisi, Bi. Elisipher Mollel.