Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali afanya mazungumzo na Kaimu Mratibu wa SADC-RCTC
                            
                                 
                                Imewekwa: 
                                31 May, 2023
                            
                        
                    
                        Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa akiwa katika picha ya pamoja na Kanali Mumbi Mulanga, Kaimu Mratibu wa Kituo cha Kupambana na Ugaidi cha Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Africa ( SADC- RCTC) mara baada ya mazungumzo yao yaliyolenga zaidi kuhusu majukumu ya Kituo hicho ambacho Makao Makuu yake yapo Mkoani Dar es Salaam -Tanzania. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Divisheni ya Uratibu na Ushauri wa Kisheria Dkt. Gift Kweka na Maafisa Kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na SADC-RCTC) Mazungumzo hayo yamefanyika leo Mtumba Dodoma.

