Mkutano wa Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya Huduma za Kisheria kutoka katika Wizara, Mamlaka na Taasisi mbalimbali za Serikali

Mkutano wa Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya Huduma za Kisheria kutoka katika Wizara, Mamlaka na Taasisi mbalimbali za Serikali
Mkutano wa Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya Huduma za Kisheria kutoka katika Wizara, Mamlaka na Taasisi mbalimbali za Serikali ulifanyika siku ya tarehe 20 Machi, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji uliopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma. Mkutano huu uliendeshwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi ambapo pamoja na mengine mada mbalimbali zinazohusu maswala ya kisheria zilijadiliwa.
Mkutano huo ni utangulizi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali wa Tanzania wa Mwaka 2024 ambao utafanyika tarehe 21 Machi, 2024 huku ukifuatiwa na uchaguuzi Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali utakaofanyika tarehe 21 Machi, 2024.