MIKATABA ITAPELEKWA BUNGENI KWA MUJIBU WA MATAKWA YA KISHERIA-AG FELESHI

MIKATABA ITAPELEKWA BUNGENI KWA MUJIBU WA MATAKWA YA KISHERIA-AG FELESHI
Na Mwandishi wetu
Dodoma
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi amelihakikishia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba, Mikataba ile ambayo inatakiwa kuridhiwa na Bunge itapelekwa katika chombo hicho kwa mujibu wa matakwa ya kisheria.
Ameyasema hayo hivi karibuni wakati alipokuwa akichangia na kujibu michango iliyotolewa na wabunge baada ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndubaro ( Mb). Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake katika Bunge la 12, Mkutano wa 7 wa Bunge la bajeti, Kikao cha 14.
“Mhe. Spika, ninao wajibu mahususi wa mambo yanayohusu mikataba, wajibu wa kwanza, ni kwa ile mikataba inayotakiwa kuridhiwa na Bunge hili, kwa mujibu wa Ibara ya 63 Ibara ndogo ya 3 (e). Ofisi yangu itaendelea kuhakikisha Mikataba inayotakiwa kuletwa na kuridhiwa na bunge inaletwa kwa kufuata matakwa ya Katiba na sheria zetu”
Akitolea ufafanuzi zaidi kuhusu suala hilo la mikataba na ambalo liliibuliwa na baadhi ya wabunge, AG Feleshi ameliambia Bunge hilo. “ Tunapoongelea masuala ya mikataba, mikataba yote inayofuata sheria inaoongozwa na sheria na kwa ushiriki wa Bunge hilo.
Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amesema, katika utekelezaji wa wajibu huo wa kuwasilisha Mikataba bungeni, hajaona kama kuna lalamiko la mikataba inayotakiwa kuletwa bungeni haijaletwa.
Akawakumbusha wabunge kwamba, wanaowajibu wa kuisimamia Serikali kupitia Kamati za Bunge hilo tukufu kamati ambazo zinasimamia Wizara na kila Taasisi ya Serikali.
Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu, Kamati hizo zina wajibu pamoja na mambo mengine, wajibu wa kutembelea miradi kule ilipo ambako kazi zinaendelea. “Na kazi hiyo ni pamoja na kujua takwa la mikataba ya miradi hiyo. Kwa hiyo niamini kwamba Bunge hili na kamati zake litaendelea kuhakikisha zile Kamati zinapewa fursa za kuwianishia miradi iliyopo na mikataba husika”
Aidha amesema, kwa zile Kamati za Bunge zinazosimamzia utendaji wa Serikali, kuliko na mikataba hiyo , zimenyimwa fursa ya kujua mikataba hiyo ina nini, ukiacha mikataba inayoletwa hapa Bungeni , basi serikali ipo tayari +kupokea hoja kama kuna ukiukwaji huo na kushughulikia.