MENEJIMENTI YAKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO JIPYA LA OMMS

Na Mwandishi wetu
Mji wa Serikali, Mtumba
Menejimenti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikiongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa
Mei 16 walitembelea , kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Jengo hilo lenye umbo la herufi Y litakalo kuwa na gorofa tano linajengwa mkabala ya Ofisi za sasa za OMMS zilizopo katika Mji wa Serikali -Mtumba Jijini Dodoma.
Timu ya Menejimenti ilipatiwa maelezo ya hali ya ujenzi ambapo Mhandisi Evans Mwingizi alieleza kwamba licha ya jengo hilo kuwa na mwonekano tofauti na majengo mengine ya wizara mbalimbali yanayoendelea kujengwa katika Mji huu wa Serikali, Jengo la OMMS litakuwa jengo kubwa na lenye majengo matano kwa pamoja.
Akizungumzia kuhusu ujezi Mhandisi Mwingizi alisema kazi inakwenda vizuri licha ya changamoto mbalimbali walizopata wakati wa kipindi cha mvua na mabadiliko ya mchoro kwa kuongeza Lift , kwa sasa kazi inaendelea vizuri.
Kwa upande wao Mejejimeti ilielezea kuridhishwa kwake na mwenendo mzima wa ujenzi wa Jengo hilo jipya
Jengo hilo linajengwa na kampuni ya Ujenzi ya SUMA JKT. Mradi mzima utagharimu shilingi Bilioni 28.6
Ujenzi huo unatarajia kuchukua miezi 24.