MAKABIDHIANO YA TUZO YA KUWA TAASISI YA PILI USIMAMIZI WA UTAWALA NA RASLIMALI WATU

Na Mwandishi Maalum
Itakumbukwa katika Mkutano wa Kazi wa Wakuu wa Idara za Utawala na Raslimali Watu uliofanyika Mkoani Arusha hivi Karibuni. Pamoja na mambo mengine, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama Taasisi inayojitegemea ilishinda Tuzo kwa kuwa mshindi wa pili wa Taasisi bora inayojitegemea inayofanya vizuri katika kusimamia utawala na raslimali watu
Leo Jumanne Octoba 17/2023 Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi amekabidhiwa rasmi Tuzo hiyo katika hafla fupi iliyofanyika Ofisini kwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma
Kabla ya MMS kukabidhiwa Tunzo hiyo, Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Silas Marwa alimkabidhi Tuzo hiyo Kaimu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Onorius Njole ( Kama Mkuu wa Utawala na Raslimali watu) na kisha naye Kumkabidhi Mkuu wa Taasisi Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa Tuzo hiyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Feleshi Pamoja na kuipongeza Idara ya Utawala na Raslimali watu na watumishi wote wa OMMS, amesema Tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa OMMS na kutaka kazi njema inayofanywa na Taasisi kuendelea kudumishwa ili kupata Tuzo nyingi Zaidi
17/10/2023