JOPO LA ITHIBATI YA WAENDESHA MARIDHIANO, UPATANISH, USULUHISHI NA MAJADILIANO LAFANYA KIKAO CHAKE

Na Mwandishi wetu
Jopo la Ithibati ya waendesha maridhiano, majadiliano, upatanishi na usuluhishi limekutana chini ya Uenyekiti wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi.
Jopo hilo limekutana siku ya Jumatano ( January 11,2023) katika ukumbi wa Mikutano uliopo katika Kituo Jumuishi ,Mahakama Kuu Kanda Morogoro ambapo lilipitia, kujadili kupitisha ama kutopitisha maombi kutoka kwa waombaji kadhaa walioomba kutoa huduma za maridhiano, majadiliano, upatanishi na usuluhishi.
Jopo linaundwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambaye ni Mwenyekiti wajumbe wakiwa ni Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniface Luhende, Rais wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea Prof. Edward Hosseah, Bi. Anita Malawo kutoka Baraza la Taifa la Ujenzi na Bi. Madeline Kimei Rais wa Taasisi ya Wasuluhishi Tanzania. Katibu wa Jopo hilo ni Wakili wa Serikali Mkuu Abdulrahman Mshamu Kutoka Wizara ya Katiba na Sheria.
Jopo la Ithibati ya waendesha maridhiano, majadiliano, upatanishi na usuluhishi hukutana mara nne kwa mwaka kupitia maombi ya waombaji zikiwamo Taasisi zinazojihusisha na utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala
Waombaji wanaopitishwa baada ya kukidhi vigezo majina yao hupelekwa kwa Msajili wa Watoa Huduma, Wizara ya Katiba na Sheria ambako hupatiwa usajili
Takribani waombaji 494 zikiwako Taasisi wamesajiliwa kuwa waendeshaji wa maridhiano, majadiliano, upatanishi na usuluhishi.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano
January 14, 2023