JAJI MKUU AISIFU OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KWA KUTAFSIRI SHERIA

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 5 Julai 2024 ametembelea banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali lililoko kwenye maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Akiwa bandani hapo Mhe. Jaji Mkuu alisifu jitihada za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu za kuamua kutafsiri sheria mbalimbali na kuwa lugha ya Kiswahili huku akitaka ufafanuzi kama baada ya tafsiri sheria zitakuwa zinapatikana kwa lugha ya kiswahili na kingereza.
"Niwapongeze kwa kutafsiri sheria kutoka kingereza kuwa kiswahili, zitakuwa zinapatikana kwa lugha ya kiswahili na kingereza?" Alimaliza kwa kuuliza Mhe. Jaji.
Akitoa maelezo kwa Mhe Jaji Mkuu wa Tanzania, Wakili Mwandamizi wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu w Serikali Bi. Angella Kimaro alisema sheria hizo zitapatikana kwa lugha ya kiswahili na kingereza.
"Sheria hizi Mhe. Jaji zitapatikana kwa lugha zote mbili kupitia mifumo yetu, pia katika wananchi watapa kuziona sheria zilizofanyiwa marekebisho kupitia madirisha yaliyoko kwenye mifumo yetu". Alisema Bi. Angella