HABARI PICHA
Imewekwa:
04 Jun, 2025

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari akiwasilisha mada wakati wa Mafunzo kwa Mawakili wa Serikali yanayoendeshwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Jijini Arusha.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali amefanya Wasilisho hilo leo tarehe 4 Juni, 2025 ambapo amewasilisha mada kuhusu "MBINU ZA KUFANYA MAJADILIANO YA MIKATABA KWA MAWAKILI WA SERIKALI NA NAMNA YA KUUNGANISHA UTAALAMU WA KISHERIA NA UJUZI WA BIASHARA"
Mafunzo hayo kwa Mawakili wa Serikali yalianza tarehe 2 Juni, 2025 na yanatarajia kukamilika tarehe 4 Juni, 2025.