HABARI PICHA
Imewekwa:
24 Mar, 2025

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Samweli M. Maneno amehudhuria kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilichofanyika tarehe 24 Machi, 2025 Bungeni Jijini, Dodoma.
Kikao hicho kilikuwa na lengo la kuchambua Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Katika hicho, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameambatana na Mwandishi Mkuu wa Sheria, Bw. Onorius Njole, Wajumbe wa Menejimenti na Watumishi wa Ofisi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.