HABARI PICHA

Imewekwa: 23 Aug, 2025
HABARI PICHA

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari ameshikiri hafla ya utiaji saini Makubaliano ya nyongeza kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni ya Nyanzaga Mining Company Limited kwa Ajili ya Uchimbaji Mkubwa wa Madini ya Dhahabu.

Hafla hiyo imefanyika tarehe 20 Agosti, 2025 katika Kijiji cha Sotta Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza, ambapo Mkataba wa nyongeza kutoka asilimia 16 hadi 20 za umiliki wa hisa za kampuni ya Ubia ya Sotta umesainiwa. 

Aidha, mradi huo utagharimu zaidi ya shilingi trilioni 1 na kuufanya kuwa mgodi mkubwa wa Dhahabu kuanzishwa tangu Mwaka 2009.

 Kusainiwa kwa mkataba huo ni matunda ya juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuweka mazingira wezeshi ya Uwekezaji.