HABARI PICHA 

Imewekwa: 14 Jul, 2025
HABARI PICHA 

Ujumbe kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel M. Maneno wamekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna na baadhi ya  Wafanyakazi wa Benki hiyo, mazungumzo baina ya Taasisi hizo yamelenga  kubadilishana uzoefu katika eneo la Huduma kwa Wateja.

Ujumbe huo umekutana na Benki hiyo tarehe 14 Julai, 2025 katika Makao Makuu ya Benki ya NMB Jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alimbatana na Mkurugenzi Msaidizi Uratibu Bw. Ipyana Mlilo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi. Leila Muhaji, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bw. Juma Mziray na Wakili wa Serikali Bw. Nyamhanga Nyamhanga