BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

YALIYOJILI KWA UFUPI WASILISHO LA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
Na Mwandishi wetu
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wake wa Kumi na Moja , Kikao cha kumi na Tano kilichoketi leo jumanne (Aprili 25/2023) limepitisha Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria.
Katika kikao hicho Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) aliliomba Bunge kuidhinisha jumla ya Shilingi Bn 383,619,511,000 kwaajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo.
Kiasi hicho cha fesha kiliombwa na kupitishwa na Bunge ni kwaajili ya Wizara na Taasisi zake Nane (8).Mafungu hayo ni Fungu 12 ambalo ni la Tume ya Utumishi wa Mahakama, Fungu 16 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Fungu 19 Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na Fungu 35 Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Mafungu mengine ni Fungu 40 Mfuko wa Mahakama, Fungu 41 Wizara ya Katiba na Sheria ( RITA/LST) Fungu 55 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Fungu 59 Tume ya Kurekebisha Sheria.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Fungu 16 imetengewa kiasi cha Bn 18,817,867,000.00 kwa mchanganuo ufuatano
Matumizi ya Misharaha ni Bn 4,072,737,000.00
Matumizi ya Mengineyo Bn 12,290,130,000.00
Matumizi mengineyo ( Ndani) Bn2,000,000,00.
Matumizi mengineyo ( Nje) sh 455,000,000.00
Aidha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi alijibu na kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa na Waheshimiwa Wabunge
Hotuba ya Bajeti inapatikana katika Wavuti ya Ofisi