HAFLA YA MAKABIDHIANO YA VIFAA VYA TEHAMA KWA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA NA TAASISI ZAKE.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb) akikabidhi vifaa vya TEHAMA kwa Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake. Hafla hiyo imefanyika leo 15 Disemba, 2025 katika Ofisi ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mtumba Dodoma.
Kwa upande wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, vifaa hivyo vya TEHAMA vimepokelewa na Bi. Faith Minani Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu kwa niaba ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

