TANGAZO LA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA CHAMA CHA MAWAKILI WA SERIKALI (PBA), 2025
Kufuatia kutangazwa kwa Tarehe ya Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali, Uongozi wa Chama cha Mawakili wa Serikali uliteua Kamati ya Uchaguzi ili kuratibu na kusimamia Uchaguzi wa Viongozi wa Chama. Kamati ya Uchaguzi inawatangazia Wanachama wote wa Chama cha Mawakili wa Serikali kuwa kutakuwa na Uchaguzi wa Viongozi wa Chama kwa nafasi zifuatazo-
- Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali;
- Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali;
- Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mawakili wa Serikali;
- Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mawakili wa Serikali;
- Katibu wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mawakili wa Serikali;
- Mweka Hazina wa Chama cha Mawakili wa Serikali; na
- Wawakilishi wa Mikoa
Wanachama wenye sifa wanashauriwa kuomba nafasi hizo kwa kujaza fomu na kuziwasilisha kwa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi zikiwa zimesainiwa ipasavyo na Mgombea pamoja na Wadhamini. Fomu hizo zinapatikana katika tovuti ya Chama na Tovuti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa vikoa vya www.tpba.go.tz na www.oag-mis.go.tz. Fomu zilizojazwa kikamilifu zitumwe kwa l.ringia@bunge.go.tz na nakala kwa rashid.said@osg.go.tz . Mwisho ya kurudisha fomu ni siku ya Ijumaa tarehe 20 Machi, 2025 saa 5.59 usiku.
Uchaguzi wa viongozi wa Kitaifa (1-6 hapo juu) utafanyika siku ya tarehe 15 Aprili, 2025 na Uchaguzi wa Wawakilishi wa Mikoa utafanyika katika Mikoa husika katika siku na tarehe kama inavyoonekana kwenye Ratiba ya Uchaguzi wa Mikoa ambayo imetolewa na Kamati ya Uchaguzi.
Sifa zinazotakiwa ili kuweza kuteuliwa kugombea ni kuwa mwanachama hai uliyesajiliwa katika Daftari la Mawakili wa Serikali na kulipa Ada ya Uanachama kwa mwaka husika wa uchaguzi pamoja na sifa nyingine zilizoanishwa katika Kanuni za Usimamizi na Uendeshaji wa Chama cha Mawakili wa Serikali T.S. Na. 529 la Mwaka 2019.
Kwa maswali na ufafanuzi wasiliana na Kamati ya Uchaguzi kupitia barua pepe l.ringia@bunge.go.tz, rashid.said@osg.go.tz au simu namba 0714560460 au 0628928553.
Hilda Kabisa
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi