HABARI PICHA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) akipata maelezo kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoka kwa Wakili wa Serikali wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Mwema Punzi wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) tarehe 16 Juni, 2025 Jijini Dar Es Salaam.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inashiriki katika Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) kwa kutoa huduma za Ushauri wa Kisheria, Elimu ya Sheria, Utatuzi wa Migogoro na Kushughulikia Malalamiko.
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) Jijini Dar es Salaam imezinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) na inafanyika kuanzia leo tarehe 16 hadi 25 Juni, 2025.