HABARI PICHA

Imewekwa: 08 Jul, 2025
HABARI PICHA

Mwandishi Mkuu wa Sheria, Bw. Onorius Njole tarehe 6 Julai 2025  ametembelea banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Maonesho ya Biashara ya 49 ya  Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Mwandishi Mkuu wa Sheria  alipokelewa na Mkurugenzi wa Divisheni ya Uratibu na Ushauri wa Kisheria Bi. Neema Ringo. 
 
Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali liko katika Mtaa wa Media, Hema la Jakaya Kikwete banda namba 24.

Maonesho ya Sabasaba yenye kauli mbiu ya "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Fahari ya Tanzania"yalianza tarehe 28 Juni , 2025 na yanatarajiwa kumalizika tarehe 13 Julai, 2025.